IQNA

Walioambukizwa corona Saudia waongezeka, Uturuki yasema Saudia inaficha ukweli

22:05 - March 27, 2020
Habari ID: 3472608
TEHRAN (IQNA)- Idadi ya walioambukizwa ugonjwa wa COVID-19 au corona nchini Saudi Arabia wanazidi kuongezeka huku Uturuki ikiituhumu Saudia kuwa inaficha ukweli kuhusu idadi kamili ya walioambukizwa.

Kwa mujibu wa taarifa, hadi kufikia leo walioambukizwa COVID-19 nchini Saudia ni 1104 baada ya kubainika kesi 92 mpya.

Wizara ya Afya ya Saudia imesema kesi 82 kati ya zilizotangazwa leo ni za walio waliogusana moja kwa moja na wagonjwa wa COVID-19 na 10 waliosalia ni wasafiri waliofika nchini humo kutoka nchi za kigeni na wote sasa wamewekwa karantini.

Wakati huo huo, Uturuki imeituhumu Saudi Arabia kuwa inaficha idadi ya wati walioambukizwa corona na jambo hilo ni kikwazo katika jitihada za kimataifa za kuzuia kuena ugonjwa huo.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki Suleyman Soylu amesema kesi za kwanza za walioambukizwa corona Uturuki zilibainika baada ya waliorejea kutoka Ibada ya Umrah Saudi kupimwa.

Amesema Saudia haikuifahamisha Uturuki au dunia kuhusu kesi hizo za corona.  Wataalamu wengi wanatilia shaka takwimu zinazotolewa na Saudia kuhusu corona huku wakiamini kuw idadi ya walioambukizwa katika ufalme huo ni kubwa zaidi ya wanaotangazwa rasmi.

Wakati huo huo siku ya Alhamisi wakuu wa Saudia walitangaza kufunga kikamilifu miji mitakatifu ya Makka na Madina ili kuzuia kuenea corona.

3887698

captcha