IQNA

Uwezekano wa kufutwa Sala ya Tarawih Saudia kutokana na corona

14:24 - April 11, 2020
Habari ID: 3472655
TEHRAN (IQNA) – Afisa mmoja wa kidini nchini Saudi Arabia amesema kuna uwezekano mkubwa kuwa Sala ya tarawih haitasaliwa katika misikiti ya nchi hiyo ili kuzuia kuenea ugonjwa wa corona au COVID-19 nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa, Mohammad al Aqil, afisa mwandamizi wa Wizara ya Masuala ya Kiislamu Saudi Arabia  katika mahojiano na Televisheni ya Al Saudiya katika kujibu swali kuhusu iwapo kusitishwa kwa sala za jamaa misikiti pia kutahusisha sala ya Tarawih katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani amesema:  “Maadamu hakuna amri kutoka baraza kuu la ulamaa na taasisi husika kuhusu kuondoa marufuku ya sala za jamaa, basi marufuku ya sala za jamaa itaendelea.”

Naye Ahmad al Mansouri, mjumbe wa mkuu wa masuala ya Harameini (Misikiti Miwili Mitakatifu ya Makka na Madina) ametoa kauli kuhusu sala katika maeneo hayo mawili matakatifu na kusema:  “Kamati  kuu itafanya tathmini  kuhusu kuswaliwa Sala ya tarawih katika Msikiti Mtakatifu wa Makka katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.”

Hadi kufikia Jumamosi 10 Aprili, watu 3,651 walikuwa wameambukizwa corona nchini Suadia Arabia na miongoni mwaka 47 wameaga dunia.

3890649

captcha