IQNA

Hilali Nyekundu ya Uturuki kuwasaidia Waislamu milioni 10 Mwezi wa Ramadhani

15:33 - April 17, 2020
Habari ID: 3472674
TEHRAN (IQNA) – Shirika la Hilali Nyekundu la Uturuki limetangaza mpango wa kuwasaidia Waislamu 10 nchini Uturuki na maeneo mengine duniani katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Akizungumza katika kongamano kwa njia ya video, Mkuu wa Hilali Nyekundu ya Uturuki, Kerem Kinik amesema: “Mwaka huu, kinyume na miaka iliyopita,  tunawasaidia watu wendi ndani ya Uturuki ambao wamekumbwa na hali mbaya kutokana na janga la corona.”

Pamoja na hayo, amesema shirika hilo litaendelea kutoa misaada kwa Waislamu kote duniani ambao wanakumbwa na umasikini, vita na majanga ya kimaumbile.

Amebaini kuwa,  Hilali Nyekundu ya Uturuki itafikisha misaada ya Ramadhani kwa watu nusu milioni katika nchi 16 duniani zikiwemo  Bosnia na Herzegovina, Bulgaria, Jamhuri ya Uturuki ya Cyprus Kaskazini, Palestina, Syria, Iraq, Sudan Kusini, Somalia, Afghanistan, Pakistan, Bangladesh, mkoa wa Rakhine nchini Myanmar, na Senegal.

Mwezi Mtukufu wa Ramadhani unatazamiwa kuanza 24 au 25 Aprili kwa kutegemea mwezi mwandamo.

Mwaka jana Hilali Nyekundu ya Uturuki ilituma misaada katika nchi 38 na maeneo 400 ndani ya Uturuki katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kinik amesema bajeti yao ya mwezi  Mtukufu wa Ramadhani mwaka huu ni dola milioni 30.

3891967

captcha