IQNA

22:51 - April 20, 2020
Habari ID: 3472683
TEHRAN (IQNA)- Rais Bashar la Assad wa Syria leo amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif mjini Damascus ambapo wamejadili masuala mbalimbali ya pande mbili, kieneo na kimataifa.

Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni matukio ya hivi karibuni ya kisiasa na vita dhidi ya ugaidi nchini Syria.

Baadhi ya duru zinasema kuwa, moja ya mada kuu katika mazungumzo ya Rais Bashar al-Assad na Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran ni kuhusiana na duru ijayo ya mazungumzo ya Astana ambayo ni maalumu kwa ajili ya kujadili kadhia ya Syria.

Duru ijayo ya mazungumzo ya Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran, Russia na Uturuki ambao ndio wadau wakuu mazungumzo hayo inatarajiwa kufanyika Jumatano ijayo.

Akiwa mjini Damascus, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alikutana na kufanya mazungumzo pia na Walid al-Muallim Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Syria.

Maandamano ya kupinga serikali yalianza nchini Syria tarehe 15 Machi 2011 kwa sura ya kufuata mkumbo wa yale yaliyokuwa yakijiri katika nchi zingine za Kiarabu. Hata hivyo tofauti kubwa zaidi kati ya matukio ya Syria na yaliyotokea katika nchi nyingine za Kiarabu ni kwamba, malalamiko ya upinzani wa ndani nchini Syria yaligeuka kuwa vita kati ya mfumo wa utawala wa nchi hiyo na makundi ya kigaidi, kutokana na uingiliaji wa mhimili wa pande nne za Wamagharibi, Waarabu, Waebrania na Waturuki.

3892972/

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: