IQNA

IRGC imerusha satalaiti iliyoandikwa aya ya Qurani Tukufu

Satalaiti ya kwanza ya kijeshi ya Iran yarushwa kwa mafanikio katika anga za mbali

14:33 - April 22, 2020
Habari ID: 3472691
TEHRAN (IQNA)- Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limerusha kwa mafanikio satalaiti ya kwanza ya kijeshi ya Iran katika anga za mbali.

Kwa mujibu wa tovuti ya Sepah News, Jeshi la IRGC limetumia kombora la kubeba sataliti la Qased kurusha katika anga za mbali sataliti hiyo inayojulikana kama Nour-1. Oparesheni ya kurusha satalaiti hiyo imetekelezwa katika eneo la jangwani la Dasht-e-Kavir kati mwa Iran.  Kwa mujibu wa taarifa satalaiti hiyo imerushwa  katika anga za mbali katika umbali wa zaidi ya kilomita 425 kutoka sayari ya dunia. Kombora hilo la kurushia satalaiti pia katika upande mmoja limeandikwa sehemu  ya aya ya 13 ya Suuratul Azzukhruf ya Qu'rani Tukufu inayosema:...

سُبْحَانَ الَّذِي سَخَّرَ لَنَا هَٰذَا وَمَا كُنَّا لَهُ مُقْرِنِينَ

"Ametakasika aliye mfanya huyu atutumikie, na tusingeliweza kufanya haya wenyewe."

Sataliti hiyo imerushwa katika anga za mbali na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu wakati jeshi hilo linaadhmisha mwaka wa 41 tokea kuasisiwa kwake mnamo Aprili 22 mwaka 1979.

Kurushwa satalaiti hiyo ya kijeshi katika anga za mbali ni tukio la kihistoria kwa sekta ya anga za mbali nchini Iran.

Iran ilirusha katika anga za mbali satalaiti yake ya kwanza kabisa inayojulikana kwa jina la Omid (yaani Tumaini) mwaka 2009. Iran pia imetangaza kuwa, katika kipindi cha miaka michache ijayo itatuma mwanaadamu katika anga za mbali. Tayari mazoezi yameshafanyika kuhusiana na lengo hilo kwa kutumwa nyani hai katika anga za mbali ambaye alirejea ardhini akiwa salama.

Mafanikio haya ya Iran katika sekta ya anga za mbali yamepatikana licha ya kuwepo vikwazo vya kila upande vya nchi za Magharibi, hasa Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kislamu.

3893356/

captcha