IQNA

Iran yalaani uamuzi wa Ujerumani wa kupiga marufuku Hizbullah

17:36 - May 01, 2020
Habari ID: 3472721
TEHRAN (IQNA)- Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani hatua ya chuki ya serikali ya Ujerumani ya kuiita Harakati ya Hizbullah ya Lebanon kuwa ni kundi la kigaidi na kusema kwamba, uamuzi huo unahudumia malengo ya utawala haramu wa Israel na Marekani.

Katika taarifa, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya IranSayyid Abbas Mousavi amesema wazi kuwa, inaonekana baadhi ya madola ya Ulaya yanachukua maamuzi na misimamo yao bila ya kuzingatia uhalisia wa mambo ulivyo katika eneo la Asia Magharibi.

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amebainisha kuwa, uamuzi huo wa serikali ya Ujerumani kwa hakika ni kuivunjia heshima serikali ya Lebanon, kwani Hizbullah ni sehemu rasmi na halali ya serikali ya Beirut na daima imekuwa ni harakati yya kisiasa yenye taathira kubwa katika uthabiti wa kisiasa wa nchi hiyo ya Kiarabu.

Amesema, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon ilikuwa na nafasi na mchango mkubwa mno katika kupambana na ugaidi wa kundi la Daesh au ISIS.

Aidha Abbas Mousavi amesema kuwa, serikali ya Ujerumani inapaswa kutoa majibu ya taathira hasi za uamuzi wake huo katika kupambana na makundi ya kweli ya kigaidi.

Jana Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ujerumani ikiwa na lengo la kuifurahisha na kuiridhisha Marekani na utawala haramu wa Israel iliitangaza Hizbullah ya Lebanon kuwa ni kundi la kigaidi na ikatangaza kupiga marufuku harakati za Hizbullah katika ardhi ya nchi hiyo ya bara Ulaya.

3471314

captcha