IQNA

Maonyesho ya Qur'ani Tukufu

Baraza la Kuunda Sera za Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran Lakutana

17:00 - January 04, 2023
Habari ID: 3476356
TEHRAN (IQNA) - Kikao cha baraza la kutunga sera za Maonyesho ya 30 ya Kimataifa ya Qur'ani Tehran kilifanya mkutano mapema wiki hii, afisa mmoja alisema.

Ali Reza Moaf, Naibu wa Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu anayesimamia masuala ya Qur'ani na Etrat ameiambia IQNA kwamba waziri wa utamaduni na baadhi ya wajumbe waandamizi wa jumuiya ya Qur'ani ya Iran walihudhuria kikao hicho.

Alisema washiriki walisisitiza haja ya kuimarisha sehemu ya kimataifa ya maonyesho hayo katika toleo lijalo.

Kwa hivyo, katika mkutano wa video na waambata wa kitamaduni wa Iran katika nchi 21 ulifanyika ambapo iliamuliwa kwamba uwezo wa vituo hivyo utumiwe na sekretarieti ya maonyesho hayo, alisema.

Kulingana na Moaf, katika kikao hicho pia ilisisitizwa kwamba uwezo wa wizara za serikali na vyombo vingine vinavyoweza kutumika katika kufanya maonyesho hayo unapaswa kufafanuliwa.

Kuzingatia zaidi sehemu ya watoto na vijana na shughuli na programu za wanawake katika maonyesho ya Qur'ani ni miongoni mwa mambo mengine yaliyosisitizwa katika mkutano huo, aliendelea kusema.

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran kila mwaka huandaliwa na Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Maonyesho hayo yanalenga kukuza fikra za Qur'ani na kuendeleza shughuli za Qur'ani nchini Iran na dunia nzima kwa ujumla.

Maonyesho hayo pia ni jukwaa la kuonyesha mafanikio ya hivi punde zaidi ya Qur'ani nchini Iran na pia bidhaa mbalimbali zinazotolewa kwa ajili ya kutangaza Kitabu hicho Kitakatifu.

Mnamo 2020 maonyesho hayo yalisitishwa na mnamo 2021 yalifanyika kwa sababu ya vizuizi vya corona nchini Iran.

Baada ya janga hilo kupungua, hafla hii ya Qur'ani ilifanyika katika ukumbi  tena mnamo Aprili 2022 na kauli mbiu ya "Quran, Kitabu cha Matumaini na Utulivu".

 

4112070

Habari zinazohusiana
captcha