IQNA

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani Tehran yaakhirishwa

19:06 - March 06, 2020
Habari ID: 3472536
TEHRAN (IQNA) - Maonyesho ya 28 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran ambayo yalikuwa yafanyike katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani yameakhirishwa kutokana na kuenea kirusi cha Corona nchini Iran.

Hayo yamesemwa na Abdul Hadi Faqihizadeh, Naibu Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Iran anayesimamia masuala ya Qur'ani na Itrah ambaye katika mahojiano na IQAN ameongeza kuwa kwa sasa haiwezekani kuandaa maonyesho hayo katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka huu kama ilivyopangwa. Amesema uamuzi kuhusu siku ya kufanyika maonyesho hayo utatangazwa baadaye. Maonyesho hayo ya kimataifa ya Qur'ani yalikuwa yaanze Mei 2 katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran huandaliwa kila mwaka na Wizara ya Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Iran na hufanyika katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Maonyesho hayo yanalenga kustawisha ufahamu na utamaduni wa Qur'ani Tukufu nchini Iran. Katika maonyesho hayo huwa kunaonyeshwa mafanikio yaliyofikiwa na Iran na nchi zingine duniani katika sekta ya Qur'ani Tukufu.

3883232

captcha