IQNA

Maonyesho ya Qur'ani

Mkuu wa Sekretarieti ya Kudumu ya Maonyesho ya Qur'ani ya Iran ateuliwa

20:56 - February 02, 2023
Habari ID: 3476505
TEHRAN (IQNA) - Mohammad Mehdi Aziz-Zadeh ameteuliwa kuwa mkuu wa sekretarieti ya kudumu ya Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran.

Aliteuliwa kushika wadhifa huo katika kikao cha Baraza la Kutunga Sera la Maonesho ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran baada ya kupata idhini ya wajumbe hao, ambayo iliidhinishwa na Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu Mohammad Mehdi Esmaeili.

 Esmaeili alitoa wito kwa Aziz-Zadeh kutumia kikamilifu uwezo wa wananchi kuandaa maonyesho ya Qur'ani, ikiwa ni pamoja na Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran, ambayo yanapangwa kufanyika katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Vile vile amemtaka mkuu mpya wa sekretarieti hiyo kufanya juhudi kwa ajili ya kuinua ubora na kuongeza ufanisi wa maonyesho ya Qur'ani na kuandaa njia ya uzalishaji na maonyesho ya bidhaa bora za Qur'ani.

Sekretarieti ya kudumu imeundwa na baraza la kutunga sera na kwa agizo la Waziri wa Utamaduni. Mkuu wa sekretarieti hiyo ambaye anashikilia wadhifa huo kwa muda wa miaka mitatu ndiye anayesimamia uandaaji wa maonesho ya Qur'ani ya kitaifa na kimataifa nchini Iran pamoja na maonyesho ya Qur'ani nje ya nchi kwa ushirikiano na Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu (ICRO).

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran kila mwaka huandaliwa na Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Maonyesho hayo yanalenga kukuza ufahamu wa Qur'ani na kuendeleza shughuli za Qur'ani.

Aidha maonyesho hayo huwasilisha mafanikio ya hivi punde zaidi ya Qur'ani nchini Iran na pia bidhaa mbalimbali zinazotolewa kwa ajili ya kutangaza Kitabu hicho Kitakatifu.

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha