IQNA

Misikiti ya London kuadhini kupitia vipaza sauti kutokana na COVID-19

11:14 - May 10, 2020
Habari ID: 3472752
TEHRAN (IQNA) – Misikiti ya London Mashariki nchini Uingereza imeanza kuadhini kupitia vipaza sauti katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili kuwasaidia Waislamu wajihisi kufungamana na misikiti ambayo imefungwa kwa muda kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19.

Baraza la Eneo la Waltham Forest limeiruhusu miskiti katika eneo hilo kuadhini kupitia vipaza sauti katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wakati wa Magharibi kila siku na Ijumaa adhuhuri wakati wa Sala ya Ijumaa.

Adhana hiyo katika misikiti imejumuisha ibara inayosema 'Swalini Majumbani Mwenu", kwa sababu misikiti imefungwa.

Hadi sasa ni misikiti tisa ya eneo hilo ambayo inaadhini kupitia vipaza sauti kwa lengo la kuwapa motisha Waislamu ambao wamelazimika kusalia katika majumbani mwao kipindi hiki cha janga la COVID-19.

Hadi kufikia Mei 10 watu takribani 215,000 walikuwa wameambukizwa COVID-19 nchini Uingereza na miongoni mwao 31,587 wamefariki dunia.

3471400

captcha