IQNA

19:30 - May 16, 2020
News ID: 3472770
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Siku ya Kimataifa ya Quds itaadhimishwa nchini Iran na pia Swala ya Idul FItr itaswaliwa kwa kuzingatia kanuni za afya kuhusiana na ugonjwa wa COVID-19.

Akizungumza Jumamosi, Rais Rouhani amesema Sala ya Idul Fitri itaswaliwa katika maeneo mbali mbali kote nchini.

Hatahivyho amesema kinyume na ilivyo ada Sala ya Idi haitaswaliwa katika viwanja vikubwa vya miji bali itaswaliwa katika misikiti au vituo vya kidini vya mitaa mbali mbali.

Rais Hassan Rouhani ameyasema hayo wakati alipohutubu katika Makao Makuu ya Kupambana na COVID-19  ambapo amesema maadhimisho  ya Siku ya Quds yatafanyika katika maeneo ambayo kirusi cha COVID-19 si tishio. Amesema Siku ya Kimataifa Quds itaadhimishwa ndani ya maeneo ya Swala ya Ijumaa na kwamba hakutakuwa na matembezi ya kawaida. Aidha amesema kuwa katika mji mkuu Tehran, wananchi watajitokeza mitaani wakiwa ndani ya magari yao chini ya usimamizi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).

Siku ya Kimataifa ya  Quds huadhimishwa katika Ijumaa ya Mwisho ya Mwezti Mtukufu wa Ramadhani,.

Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu hayati Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu amrehemu) ndiye aliyeipa siku hiyo ya Ijumaa ya mwisho ya mwezi Ramadhani jina la Siku ya Kimataifa ya Quds kwa shabaha ya kuakisi dhulma ya kihistoria inayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya watu wanaoendelea kudhulumiwa na kukandamizwa wa Palestina na ardhi yao takatifu. Tokea ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran mwaka 1979, Siku ya Kimataifa ya Quds imekuwa ikiadhimishwa kupitia maandamano na makongamano  kote duniani.

3899190

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: