IQNA

Mkuu wa Kamandi ya Vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Tetesi za kufika ukingoni Israel ghasibu zinasikika Tel Aviv

15:33 - May 20, 2020
Habari ID: 3472784
TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Kamandi ya Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, Intifadha ya taifa la Palestina imeshavuka mipaka ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na kuingia kwenye awamu itakayoamua hatima yake na akasisitiza kwamba: Minong'ono ya kufikia tamati Israel ghasibu inasikika kwenye mitaa ya Tel Aviv.

Meja Jenerali Mohammad Bagheri ameyasema hayo leo katika ujumbe kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Quds na akaongeza kuwa, upana wa stratejia ya mahubiri ya "muqawama wenye msingi wa Palestina" ukiwa na satua iliyosambaa katika jiografia ya Quds na ardhi iliyoizunguka umedhoofisha irada ya maghasibu wa ardhi hiyo.

Jenerali Bagheri ameongeza kuwa, Uzayuni, ambao umeiweka Palestina chini ya udhbiti wake wa kishetani kwa himaya ya Marekani na waitifaki wake makhabithi, huku ukitenda jinai mtawalia na bila kusita kwa miaka 72, leo hii umeelewa vyema kwamba wale wahusika wakuu wa kutetea dhulma na uonevu dhidi ya wananchi wa Palestina na uvamizi na ukaliaji kwa mabavu ardhi zao za jadi za mababu zao, hivi sasa, wao wenyewe wamekwama kwenye kinamasi kikubwa cha mabalaa na matatizo na wala hawana uwezo tena wa kuuhakikishia na kuudhaminia uhai wake utawala wa Kizayuni.

Mkuu wa vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, kutokana na mripuko wa virusi vya corona, maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka huu yatafanyika kwa sura na njia tofauti na akabainisha kuwa, mataifa huru yanayotetea haki na kupinga dhulma na ubeberu yatapaza sauti zao kwa azma na irada thabiti ya kutetea ukombozi wa Quds Tukufu na kwamba kutimuliwa Marekani gaidi na mtenda jinai katika eneo kutakuwa ndio utangulizi wa ukombozi huo.

Meja Jenerali Bagheri amesema, licha ya viongozi wa White House kugharimika pakubwa kwa kutumia dola trilioni tisa katika eneo, lakini hawana uwezo tena wa kupiga upatu wa vita; na akasisitiza kuwa, wananchi na vikosi vya ulinzi vya Iran wako mstari wa mbele katika kambi iliyoungana dhidi ya Uzayuni na wanatoa msaada kwa ajili ya kuikomboa Palestina.

Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka huu itakuwa ni Ijumaa ya tarehe 28 Ramadhani, 1441 Hijria inayosaidiana na Mei 22, 2020 Miladia.

3900366

captcha