IQNA

22:59 - May 25, 2020
News ID: 3472801
TEHRAN (IQNA) - Maeneo matakatifu ya ibada na ziara katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yameanza kufunguliwa baada ya kuwepo mafanikio makubwa katika kudhibiti ugonjwa wa COVID-19.

Leo Haram za Imam Ridha AS, Imam wa Nane kutoka kizazi cha Bwana Mtume Muhammad SAW huko Mash'had na Haram ya Bibi Maasuma SA, ndugu wa kike wa Imam Ridha AS iliyoko Qum, kusini mwa Tehran zimefunguliwa na kuwapokea waumini waliokuwa na hamu kubwa ya kutembelea maeneo hayo.

Haram tukufu za Mash'had na Qum zilifungwa baada ya kuanza kuenea ugonjwa wa COVID-19 Iran zimefunguliwa mara baada ya kuchomoza jua. Haram hizo zitakuwa zinafunguliwa saa moja baada ya kuchomoza jua na kufungwa saa moja kabla ya kuzama jua kila siku.. Tab'an wafanya ziara katika maeneo hayo matakatifu wametakiwa kuchunga taratibu na maelekezo yote ya watu wa afya ili kuepusha maambukizi wa COVID-19.

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran siku ya Jumamosi alipokuwa anazungumza kwenye kikao cha Kamati ya Taifa ya Kupambana na Corona, aliashiria mchakato wa kupambana na ugonjwa wa COVID-19 humu nchini na kusema, Iran imekwenda kwa utaratibu mzuri sana katika kupambana na ugonjwa huo. Imepitia vipindi vitatu hatua kwa hatua. Kipindi cha kwanza kilikuwa ni cha kutoa taarifa ya kina kuhusu ugonjwa huo, hatua ya pili ni tahadhari za wakati wa hatari wa corona na hatua ya tatu ilikuwa ni kuanza kufunguliwa pole pole maeneo mbalimbali na hivi sasa imeingia katika hatua ya nne ya kuudhibiti ugonjwa wa COVID-19.

3901211

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: