IQNA

10:34 - May 30, 2020
News ID: 3472815
TEHRAN (IQNA) - Jeshi la Polisi la utawala wa Kizayuni wa Israel Ijumaa liliwazuia Wapalestina kuswali katika Msikiti wa Haram ya Nabii Ibrahim (Amani ya Mwenyezi Mungu Iwe Juu Yake) mjini al Khalil (Hebron) katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Pamoja na kuwa Mamlaka ya Ndani ya Palestina imetangaza kuwa zuio la uongjwa wa COVID-19  limemalizika na hivyo kuruhusu misikiti na makanisa katika eneo hilo kufunguliwa, askari wa utawala wa Kizayuni wamewazuia Waislamu kuswali.

Taarifa zinasema wakati muadhini alianza kuadhini Ijumaa audhuhuri walowezi wa Kizayuni nao walianz akugonga kuta za msikiti huo na wakawataka wanajeshi wasitishea adhana hiyo.

Wakati huo huo, mwanachama wa ngazi za juu wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina amelaani vikali hatua ya utawala wa Kizayuni ya kuwazuia Waislamu Wapalestina kuingia Msikiti wa Haram ya Nabii Ibrahim mjini al Khalil (Hebron) na kusema kitendo hicho ni hujuma ya wazi.

Khader Adnan, mwanachama mwandamizi wa Jihad Islamu amesema utawala wa Kizayuni wa Israel, ambao unakalia kwa mabavu Quds Tukufu (Jerusalem) unalenga kueneza satwa yake katika Msikiti na Haram ya Nabii Ibrahim kwa kuwazuia Wapalestina kuswali katika eneo hilo takatifu. Amesema kitendo hicho cha Israel ni jinai kubwa.

Naye Fauzi Barhoum, Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS)  amesema kuwazuia Waislamu kuswali katika Msikiti wa Nabii Ibrahim mjini al Khalil ni ukiukwaji wa wazi wa haki za taifa la Palestina. Aidha amesema kimya cha jamii ya kimataifa na hatua ya baadhi ya nchi za Kiarabu kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel ni mambo ambayo yameufanya utawala huo ghasibu upate kiburi zaidi cha kuendelea kukiuka haki za Wapalestina.

Barhoum amesema sera za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina na ardhi tukufu za Palestina hazitapelekea Wapalestina kulegeza msimamo kuhusu itikadi ya mapambano na muqawama na hivyo vijana wanamapinduzi Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi watatendelea kusimama imara.

Haram ya Nabii Ibrahim ni jengo lililoko katikati mwa mji wa al Khalil umbali wa kilomita 44 kutoka Baitul Muqaddas na wafuasi wa dini zote za mbinguni wanaamini kwamba mwili wa Nabii Ibrahim (AS) umezikwa mahala hapo.

Itakumbukuwa kuwa mnamo mwezi Julai mwaka 2017, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) lilitangaza kuwa mji wa Al Khalil ulioko Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan ambao ni moja ya turathi za kimataifa unakabiliwa na hatari kutokana na sera haribifu za utawala wa Kizayuni. 

3471540

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: