Dini tatu zinazoamini Mungu mmoja za Uyahudi, Ukristo na Uislamu zinahusishwa na Ibrahim na hivyo pia hutiwa imani za Ibrahim.
Ibrahim alikuwa nabii Ulul Adhm wa pili baada ya Nuh (AS). Yeye ni babu wa Waarabu kupitia kwa mwanawe Ismail (AS) na babu wa Bani Israil kupitia kwa mwanawe mwingine Is’haq.
Manabii wa imani ya Mungu mmoja ni kizazi cha Ibrahim (AS). Na tukamtunukia (Ibrahim) Is-haq na Yaakub. Kila mmoja wao tulimwongoa. Na Nuhu tulimwongoa kabla. Na katika kizazi chake tulimwongoa Daud na Suleiman na Ayyub na Yusuf na Musa na Harun. Na hivi ndivyo tunavyo walipa wafanyao wema. Na Zakaria na Yahya na Isa na Ilyas. Wote walikuwa miongoni mwa watu wema. Na Ismail, na Al Yasaa, na Yunus, na Lut´. Na wote tuliwafadhilisha juu ya walimwengu wote. (Sura Al-Anaam: Aya 84-86)
Ndio maana anaitwa Abu Al-Anbya (baba wa Mitume.
Mama yake aliitwa Amaliya, au Youna au Awsha. Alizaliwa kati ya miaka ya 2000 na 1990 KK. Watafiti wengi wanaamini alizaliwa Susa, Babeli au ardhi ya Harran.
Ibrahim (AS) alikuwa mwanzilishi wa Al-Kaaba tukufu na ni chanzo za idadi kubwa ya mila katika imani ya tauhidi. Sura ya 14 katika Qur’ani Tukufu imepewa jina lake na katika sura 25 kuna marejeo ya maneno na matendo yake.
Katika Surah Mayram, kuna kutajwa kwa mjadala kati ya Ibrahim na baba yake. Katika Aya ya 74 ya Surah Al-Anaam, Mungu anasema alipinga ibada ya masanamu ya baba yake na akamkaribisha kwenye njia iliyonyooka, lakini kwamba baba yake, Azar, alikataa na kumtisha. Baada ya majadiliano mengi, Azar aliahidi kumwamini Mungu na Ibrahimu aliahidi kumwomba Mungu amsamehe ikiwa ataamini. Hata hivyo, Azar hakutimiza ahadi yake na Ibrahimu akajitenga naye.
Aya za 76-79 za Surah Al-Anaam zinazungumzia jinsi alivyofikia tauhidi safi baada ya kuzingatia maumbile ya ajabu ya mwezi, jua na nyota.
Kwa mujibu wa Aya ya 260 ya Surah Al-Baqarah, Ibrahim alimwomba Mungu amuonyeshe jinsi anavyowafufua wafu.
Kuna matukio mengine mawili makubwa katika maisha yake. Moja ni mijadala yake na Nemrud, mtawala wa wakati huo. Hatimaye Nemrud alimtupa kwenye moto lakini Mungu akageuza moto kuwa bustani ya maua. (Aya ya 258 ya Sura Al-Baqarah; Aya ya 68-69 ya Surah Al-Anbya); Aya ya 24 ya Surat Al-Ankabut; Aya za 97-98 za Surah Saffat)
Nyingine ni Mungu kumwamuru amtoe dhabihu mwanawe, Ismail (AS) na akaanza kutekeleza agizo hilo lakini dakika ya mwisho, Mungu alimtuma kondoo dume atolewe dhabihu na Ibrahimu akafaulu mtihani huo mkubwa aliyopewa na Mwenyezi Mungu.
Ibrahim (AS) na dini yake wameitwa Hanie (mnyofu, muumini wa kweli). Qur’ani Tukufu inasisitiza uhusiano mkubwa na wa kina wa kiroho kati ya Mtume Muhammad (SAW) na dini yake na Nabii Ibrahim (AS). (Aya ya 68 ya Surah Al Imran na Aya ya 78 ya Surah Hajj)
Ibrahimu (AS) daima amekuwa akiheshimiwa na wafuasi wa dini za Mungu mmoja.
Inasemekana aliishi kati ya miaka 170 na 200. Kaburi lake liko katika sehemu huko Palestina inayojulikana leo kama Al-Khalil.
3489275