IQNA

Wazayuni wazuia adhana mara kadhaa katika Msikiti wa Ibrahim mjini Al Khalil

17:03 - February 02, 2021
Habari ID: 3473614
TEHRAN (IQNA) - Wakuu wa Utawala wa Kizayuni wa Israel wanazuia katika Msikiti wa Nabii Ibrahim, Amani iwe juu yake, ulioko katika mji wa Al Khalil au Hebron huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Palestina, wakuu wa utawala dhalimu wa Israel wanatumia kila mbinu kujaribu kuufunga, kuuhujumu na kuuharibu msikiti huo mbali na kuzuia adhana hapo mara kwa mara.

Kwa mujibu wa ripoti ya Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini ya Palestina, katika mwezi uliopita wa januari pekee, Wazayuni walizuia adhana mara 50 katika Msikiti wa Nabii Ibarahim AS.

Wazayuni wanazuia adhana, hasa adhana ya Magharibi,  katika msikiti huo mtakatifu kwa kisingizo cha kuwa sauti ya adhana inawakera walowezi wa Kizayuni katika eneo hilo.

Njama nyingine inayotekelezwa na Wazayuni ilihatimaywe waweze kutumiza ndoto yao chafu ya kuutwaa msikiti huo ni  kuzuia kamati ya ukarabati wa msikiti huo kutekeleza shughuli zake.

Msikiti wa Ibrahim AS  uko katika kitongoji cha kale cha Al Khalil (Hebron) kusini mwa Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Kwa mujibu wa baadhi ya Hadithi, ndani ya msikiti huo kuna kaburi la Nabii Ibrahim AS na mkewe Sarah na vile vile makaburi ya Manabii Is-haq na Yaaqub AS na ya wake zao.

Itakumbukuwa kuwa mnamo mwezi Julai mwaka 2017, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) lilitangaza kuwa mji wa Al Khalil ulioko Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan ambao ni moja ya turathi za kimataifa unakabiliwa na hatari kutokana na sera haribifu za utawala wa Kizayuni. 

3951544/

captcha