IQNA

Kiongozi Muadhamu atoa mkono wa pole kufuatia kifo cha katibu mkuu wa zamani wa Jihad Islami ya Palestina

17:49 - June 08, 2020
Habari ID: 3472847
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa mkono wa pole kufuatia kuaga dunia Katibu Mkuu wa zamani wa Harakati ya Jihadu Islami ya Palestina, Ramadhan Abdullah Shalah.

Katika salamu zake za rambirambi kufuatia kuaga dunia shakhsia huyo,  Ayatullah Ali Khamenei amesema kifo cha mwanaharakati huyo wa Kipalestina kimegusa si tu Wapalestina, lakini pia wanajihadi na wanamuqawama katika sehemu mbalimbali duniani waliojitolea muhanga kwa ajili ya kadhia ya Palestina.

Kiongozi Muadhamu amesema, "muqawama wa Palestina umepoteza kiungo muaminifu na mwenye thamani kubwa na natumai kwa muongozo na msaada wa Mwenyezi Mungu, shakhsia watakaochukua nafasi zilizoachwa na mashujaa kama Fathi Shaqaqi and Ramadan Abdullah, watajaza pengo hilo."

Jana Jumapili pia, Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliashiria tukio la kuaga dunia katibu mkuu huyo wa zamani wa Jihad Islami ya Palestina na kusema kuwa, shakhsia huyo alisabilia maisha yake yote katika kupambana na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kadhalika Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hapo jana alituma salamu za rambirambi kufuatia kuaga dunia Shalah na kusema kuwa, Katibu Mkuu huyo wa zamani wa Jihad Islami ya Palestina alikuwa mtu mwenye khushuu, msomi, mwanafikra aliyekuwa na fikra za kukurubisha madhehebu za Kiislamu na aliyefahamu kwa kina matukio ya kieneo na dunia.

Ramadhan Shalah aliaga dunia Jumamosi ya juzi akiwa hospitalini katika mji wa Gaza, baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu. Mwanaharakati huyo wa Palestina alizikwa jana Jumapili katika mji mkuu wa Syria, Damascus.

3903705/

captcha