IQNA

Katibu Mkuu wa Hizbullah amuomboleza Ramadhan Abdullah

19:42 - June 09, 2020
Habari ID: 3472849
TEHRAN (IQNA) – Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sayyed Hassan Nasrallah ametuma salamu za rambi rambi kufuatia kifo cha Katibu Mkuu wa zamani wa Harakati ya Jihadi Islami ya Palestina Ramadan Abdullah Shalah.

Kiongozi wa Hizbullah ameyasema hayo Jumanne katika  katika mazungumzo ya simu na Katibu Mkuu wa sasa wa Harakati ya Jihad Islami Ziad al-Nakhala.

Katika mazungumzo hayo, Sayyed Nasrallah ametuma salamu za rambi rambi kwa watu wa Palestina na familia ya Shalah kufuatia kuaga dunia mwanamapambano huyo.

Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah Sheikh Naim Qassim naye pia ametuma salamu za rambi rambi kufuatia kuaga dunia Shalah na kumtaja kuwa mtu aliyetumia muda wake wote katika Jihadi na mapambano ya kuikomboa Palestina.

Ramadhan Abdallah Shalah, Katibu Mkuu wa zamani wa Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina aliaga Jumamosi akiwa na umri wa miaka 62 kutokana na maradhi ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.

Kifo cha Dakta Ramadhan Abdallah ni tukio chungu na la majonzi kwa taifa zima la Palestina. Pamoja na hayo hakuna shaka yoyote kwamba njia ya shakhsia huyo shupavu na mkubwa wa Palestina itaendelezwa kwa nguvu zote na shakhsia wengine wakubwa wa taifa hilo, akiwemo, Ziyad al-Nakhala, Katibu Mkuu mpya wa Jihadul Islami.

3903968

captcha