IQNA

Iran ni muungaji mkono mkubwa zaidi wa harakati za ukombozi wa Palestina

15:26 - June 26, 2021
Habari ID: 3474045
TEHRAN (IQNA)- Nasser Abu Sharif, mwakilishi wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina mjini Tehran amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni muungaji mkono mkubwa zaidi wa harakati za kupigania ukombozi wa Palestina.

Akizungumza hivi karibuni katika kongamano la "Oparesheni ya Upanga wa Quds, Palestina na Mhimili wa Muqawama; Mafanikio na Mustakabali" amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inasimama kidete kukabiliana na nchi za Magharibi na watifaki wao huku ikiunga mkono ukombozi wa Palestina.

Abu Sharif aidha amesema ushindi wa taifa la Palestina ni ahadi ya Mwenyezi Mungu ambayo bila shaka itatimia.

Ameongeza kuwa dalili za ushindi zinazidi kudhihirika wazi na mfano wa hilo ni mafanikio ya harakati za muqawama katika vita vya mwezi Mei mwaka huu ambapo makombora yalivurumishwa kutoka Ghaza kuelekea katika maeneo yaliyopachikwa jina la 'Israel' na kusababisha hasara kubwa. Amesema jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel ambalo lilikuwa likijigamba kuwa haliwezi kushindwa limepata pigo kubwa kutoka kwa wapigania ukombozi wa Palestina.

Mwakilishi wa Jihad Islami amesema mmoja kati ya matokeo ya ushindi wa Wapalestina huko Ghaza ni kuondolewa madarakani kwa madhila Benjamin Netanyahu.

Abu Sharif amebainisha masikitiko yake kuwa baadhi ya tawala za Kiarabu zimejikurubisha kwa utawala wa Kizayuni wa Israel jambo ambalo ni kinyume cha wananchi waliowengi katika nchi hizo.

3979857

captcha