IQNA

Swala ya Ijumaa kwa mara ya kwanza katika misikiti ya Scotland kwa mara ya kwanza baada ya miezi kadhaa

20:17 - July 18, 2020
Habari ID: 3472975
TEHRAN (IQNA) – Waislamu kote Scotland nchini Uingereza wameshiriki katika Swala ya Ijumaa wameshiriki katika Swala ya Ijumaa kwa mara ya kwanza baada ya miezi kadhaa baada ya misikiti kufunguwa ili kuzuia kuenea ugonjwa wa corona.

Wakuu wa afya wanasema wamweka sheria ya kuzuia kuenea ugonjwa wa corona au COVID-19 ikiwa ni pamoja na kuwashurutisha waumini wote kuvaa barakao na waumini katika msikiti wasizidi 50. Katika Msikiti wa Baitur Rahman katika Barabara ya Haugh mjini Glasgow, waumini hawakuzidi 25 nawote walipimwa kiwango cha joto mwilini kabla ya kuingia.

Aidha vyoo vya misikiti vimefungwa na pia waumini wametakiwa washike wudhuu nyumbani kabla ya kufika msikitini. Halikadhalika waumini wametakiwa wafike msikitini wakiwa na mkeka binafsi wa kuswali ili kuzuia maambukizi ya corona.

Msemaji wa jamii za Waislamu mjini Glasgow amesema Waislamu wamepata baraka tele baada ya misikiti kufunguliwa. Ameongeza kuwa msikiti ni nyumba kwa kwanza ya kila Mwislamu  na ni nyumba ya kimaanawi ambayo kufunguliwa kwake tena ni baraka kubwa. “Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupatia fursa hii ya kuweza kurejea misikitini.”

3472026

Kishikizo: scotland ، waislamu ، msikiti ، covid-19
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha