IQNA

Ripota wa kwanza Mwislamu mwenye kuvaa Hijabu huko Scotland

19:30 - August 02, 2020
Habari ID: 3473026
TEHRAN (IQNA) – Bi. Tasnim Nazeer hakudani atakuwa ripota wa kwanza Mwislamu kuonekana katika televisheni akiwa amevalia vazi la staha la Kiislamu la Hijabu huko Scotland, Uingereza.

Nazeer, ambaye ni mwenyeji wa Glasgow, alianza kuripoti katika televisehni ya STV News mapema wiki hii.

Amesema ana furaha kubwa kufanya kazi yake ya kwanza kama ripoti wa STV News ambapo ripoti hiyo imehusu kusaidia familia ambazo zimekumbwa na msiba Scotland. Amesema ana uhakika kuwa hakuna mwaname Mwislamu aliyevalia hijabu liyewahi kuripoti katika televisheni ya Scotland. "Naishukuru STV kwa kunipa fursa hii na nina furaha kuwa imeajiri kwa msingi wa ujuzi na uwezo wangu wa kufanya kazi."

Amesema ni muhimu kwa vyombo vya habari Scotland kuwa na wafanyakazi ambao wanaakisi taswira ya kitaifa ya jamii nzima ili mitazamo mbali mbali iweze kusikika.

3472168/

captcha