IQNA

Sayyid Hassan Nasrallah
18:32 - August 30, 2020
Habari ID: 3473118
TEHRAN (IQNA) – Katibu mkuu wa Harakati ya Hizbullah Sayyid Hassan Nasrallah amesema balozi za kigeni mjini Beirut zinahusika katika njama dhidi ya harakati hiyo.

Katika hotuba yake Jumamosi, katika usiku wa kuamkia Ashura, Sayyid Hassan Nasrallah alisema kwamba hujuma ya vyombo vya habari ndiyo stratijia ya sasa ya maadui dhidi ya wanamapambano ya ukombozi dhidi ya utawala haramu wa Israel na washirika wake.

Aliongeza kuwa hujuma ya vyombo vya habari dhidi ya Hizbullah imeanzishwa na kuongezwa  kwamba kumeanzishwa vituo kadhaa ambavyo vinabuni habari za uongo na kuzisambaza katika vyombo vya habari. 
Sayyid Nasrallah amesema kuwa, vita hivyo vya vyombo vya habari vinasimamiwa na kambi ya Waarabu, Wamagharibi na Wazayuni wakishirikiana na balozi zao katika nchi walengwa ikiwemo Lebanon. 
Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema kuwa balozi hizo za nchi za Kimagharibi na Kiarabu zimetumia mamilioni ya dola za Marekani kwa ajili ya kubuni na kusambaza habari za uongo na kuchafua sura ya Hizbullah katika fikra za walimwengu na kwamba, hujuma hii kubwa ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii haijawahi kushuhudiwa katika kipindi chote cha miaka 40 hadi 50 iliyopita.

Nukta ya mwisho iliyoashiriwa na Sayyid Hassan Nasrallah katika houba yake ya usiku wa kuamkia siku ya leo ya Ashura ni kwamba, ingawa harakati za mapambano na muqawama katika eneo la magharibi mwa Asia hazina nguvu kubwa ya vyombo vya habari, lakini muqawama na mapambano hayo ya ukombozi yamezaliwa na kukulia katika skuli ya Imam Hussein bin Ali AS na masahaba zake, na miongoni mwa sifa kuu za shule hiyo ni kupambana na dhulma na madhalimu. Sifa hii ndiyo sababu kuu ya kuzishinda njama za maadui dhidi ya wapigania haki na uadilifu katika kipindi chote cha miaka 38 iliyopita, yaani tangu kuanzishwa harakati ya Hizbullah ya Lebanon mwaka 1982 hadi hivi sasa.  

3472410

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: