IQNA

Sayyid Nasrallah atoa wito kwa Waislamu kutumia Muharram kujikuza kiroho

22:04 - August 21, 2020
Habari ID: 3473089
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrallah ametoa wito kwa Waislamu kujikuza kiroho, kisaikolojia na kiakili katika maombolezo ya Mwezi wa Muharram.

Sayyid Hassan Nasrullah ameyasema hayo katika hotuba kwa mnasaba wa kuanza mwezi wa Mfunguo Nne, Muharram.

Akizungumza Alhamisi  Sayyid Nasrallah aliashiria kuwadia mwezi wa Muharram na masiku ya maombolezo ya Bwana wa Mashahidi Imam Hussein (AS), Imamu wa Tatu wa Waislamu wa Kishia ulimwenguni na akasema: Watu walioshiriki kwenye mapambano ya Karbala leo hii ni ruwaza na vigezo kwetu sisi. Aidha ametoa wito kwa waumini kuzingatia kanuni za kiafya wakati huu wa maombolezo ya mwezi wa Muharram.

Kwingineko katika hotuba yake,Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema, utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ndilo tishio lenye umuhimu zaidi kwa eneo la Asia Magharibi.

Katika hotuba yake hiyo, Sayyid Hassan Nasrullah amewatolea mwito Walebanon na Waislamu kuisoma historia kwa makini na jinsi utawala bandia wa Kizayuni ulivyoundwa; na akasema: Kuijua historia ya Palestina na historia ya wavamizi waliotia mguu wao ndani ya ardhi ya Palestina ni jambo lenye ulazima kwa ajili ya kukabiliana na adui Mzayuni.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Katibu Mkuu wa Hizbullah amesisitiza kuwa, haiwezekani kwa mtazamo wa kiutambulisho, kupambanua baina ya Marekani na Israel na akafafanua kwamba, hii leo Marekani ndio changamoto kubwa zaidi kwa mataifa ya dunia na tishio kubwa zaidi kwa amani na usalama wa kimataifa.

Sayyid Hassan Nasrullah amesema, serikali ya Marekani ni utawala wa kishenzi na wa ubaguzi wa rangi na akasisitiza kuwa, serikali ya Marekani imesimama juu ya misingi ya dhulma na ubaguzi wa rangi.

Katibu Mkuu wa Hizbullah ameiashiria pia serikali ya Uingereza ambayo amesema ni kibaraka wa Wazayuni na akafafanua kuwa: London imejitolea kufanikisha malengo ya kikoloni ya Wazayuni.

3472330

captcha