IQNA

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran: Jinai za Israel dhidi ya Palestina zimechupa mipaka

17:53 - October 01, 2020
Habari ID: 3473219
TEHRAN (IQNA) – Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa taarifa na kusema jina za utawala wa Kizayuni wa Israel zimechupa mipaka.

Ikitoa taarifa yake kwa mnasaba wa Siku ya Kushikamana na Watoto wa Palestina, Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imeandika katika ukurasa wake rasmi wa Twitter kwamba kuwa, historia haiwezi kamwe kuwasamehe wauaji na wasaliti.

Taarifa hiyo imesema kwamba; "Miaka 20 nyuma, Muhammad al Durrah aliuliwa kikatili na kinyama mno tena kwa makusudi na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni akiwa pembeni mwa baba yake na hivyo kuwaonesha walimwengu ukatili uliochupa mipaka wa wavamizi wa Quds."

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imeongeza kuwa, miaka 20 baada ya ukatili na unyama huo, zimejitokeza tawala za eneo la Asia Magharibi na kuungana na wauaji wa kijana huyo mdogo wa Kipaletina; historia haiwezi kuwasamehe wauaji na wasaliti.

Wiki za hivi karibuni tawala za kiimla za nchi mbili za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Bahrain zilitangaza rasmi kuweka uhusiano wa kidiplomasia na utawala wa Kizayuni wa Israel ambao mikono yake imejaa damu za watoto wasio na hatia wa Palestina.

Tarehe 30 Septemba imepewa jina la Siku ya Kushikamana na Watoto wa Palestina katika kalenda ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ili kuubakisha hai unyama aliofanyiwa kijana mdogo wa Kipalestina Muhammad al Durrah na wanajeshi makatili wa utawala wa Kizayuni.

Tarehe 30 Septemba mwaka 2000, katika siku za awali za Intifadha ya Pili yaani Intifadha ya al Aqsa, vyombo vya habari vilirusha hewani picha za kijana wa miaka 12 wa Kipalestina, Muhammad al Durrah, ambaye alikuwa akijificha vilivyo nyuma ya baba yake ili asipigwe risasi na Wazayuni, lakini wanajeshi hao makatili walimpiga risasi kichwani na kumuua shahidi kwa makusudi ili kumuumiza zaidi baba yake na kuonyesha walivyo makatili kupita kiasi.

2360225

captcha