IQNA

20:46 - December 02, 2020
Habari ID: 3473416
TEHRAN (IQNA) - Wakuu wa Yemen wametoa tahadhari kuhusu hali mbaya ya kibinadamu inayozidi kuwa mbaya nchini humo kutokana na vita vinavyoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya nchi hiyo masikini ya Kiarabu ambapo 'mtoto mmoja wa Yemen hupoteza maisha kila dakika 10'.

Wizara ya Afya ya Yemen imetao taarifa na kuonya kuwa kupingua misaada ya kimataifa kumepelekea hali nchi Yemen kuzidi kuwa mbaya.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, lishe duni shahidi miongoni mwa watoto wa Yemen walio chini ya umri wa miaka mitano ni ya kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa katika historia.

Mwezi jana Umoja wa Mataifa ulionya kuwa Yemen inakabiliwa na baa la njaa ambalo halijawahi kuhushudiwa duniani kwa miongo kadhaa.

Jumanne pia Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) ilitangaza kuwa vita vya Saudi Arabia dhidi ya Yemen vimepelekea zaidi ya watu 233,000 kupoteza maisha katika kipindi cha miaka sita iliyopita.

Ikumbukwe kuwa mnamo mwezi Machi 2015 Saudi Arabia, ikiungwa mkono na  Marekani, Umoja wa Falme za Kiarabu  na nchi zingine kadhaa iliivamia kijeshi Yemen na kuiwekea mzingiro wa kila upande nchi hiyo.

Saudia ilianzisha mashambulizi dhidi ya Yemen mwishoni kwa lengo la kuiondoa madarakani Harakati ya Ansarullah na kumrejesha madarakani Abdrabbuh Mansour Hadi, rais wa zamani wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kukimbilia Riyadh. Hata hivyo hadi sasa Saudia na washirika wake wameshindwa kufikia malengo yao kutokana na kusimama kidete wananchi wa Yemen.

3473290

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: