IQNA

WFP yaonya kuhusu baa la njaa Yemen huku Saudia ikiendeleza vita

19:25 - November 13, 2020
Habari ID: 3473355
TEHRAN (IQNA)- Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuwa mamilioni ya watu wa Yemen, hasa wanawake na watoto, wanakabiliwa na baa la njaa huku Saudia ikiendeleza vita dhidi ya nchi hiyo masikini zaidi katika bara Arabu.

“Hivi sasa tunaelekea katika janga na maafa,” amesema Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula Duniani (WFP), David Beasley wakati alipohutubu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Umoja wa Mataifa umesema maafa ya kibinadamu Yemen ni makubwa zaidi duniani, ambapo asilimia 80 ya watu wote milioni 30 nchini humo wanahitaji msaada kutokana na vita vinavyoongozwa na Saudia dhidi ya nchi hiyo.

Saudia ilianzisha mashambulizi dhidi ya Yemen mwishoni mwa mwezi Machi 2015 kwa lengo la kuiondoa madarakani Harakati ya Ansarullah na kumrejesha madarakani Abdrabbuh Mansour Hadi, rais wa zamani wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kukimbilia Riyadh. Hata hivyo hadi sasa Saudia na washirika wake wameshindwa kufikia malengo yao kutokana na kusimama kidete wananchi wa Yemen. 

Mwezi Juni, Kituo cha Haki za Binadamu cha Ainul Insaniya kilitoa ripoti na kutangaza kuwa tokea muungano wa Saudia uanzishe vita dhidi ya Yemen mnamo Machi 26, 2015 hadi sasa watu 16, 672 wamepoteza maisha moja kwa moja kutokana na vita ambapo miongoni mwao kuna watoto 3,742 na wanawake 2,364.

3473098

Kishikizo: yemen saudi arabia njaa
captcha