IQNA

UNICEF: Yemen ni sehemu hatari zaidi kwa watoto duniani

21:03 - December 13, 2020
Habari ID: 3473453
TEHRAN (IQNA) – Yemen ni sehemu hatari zaidi kwa watoto duniani, amesema Henrietta Fore Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF).

Katika taarifa amesema nchi hiyo masikini zaidi katika Bara Arabu inaelekea kuangamia kabisa kutokana na vita ambavyo vinaongozwa na Saudi Arabia dhidi ya Wayemen.

“Zaidi ya asilimia 80 ya watu wa Yemen wanahitaji msaada wa dharara wa kibinaadamu na pia wanahitaji ulinzi. Miongoni mwao wamo watoto milioni 12 ambao maisha yao ni jinamizi la waliomacho,” amesema Fore alipohutubua katika kikao kwa njia ya intaneti.

Bi.  Fore ameongeza kuwa, Yemen ni eneo hatari zaidi kwa mototo duniani. Ameongeza kuwa: “Mtoto mmoja hufariki Yemen kila dakika 10 kutokana na magonjwa yanayoweza kuepukika. Watoto milioni mbili hawaendi shuleni na maelefu yaw engine wameuawa, kujeruhiwa au kutumiwa kama wapiganaji tokea mwaka 2015.” Ametoa mfano na kusema wiki iliyopita watoto 11 waliuawa, akiwemo motto mchanga wa mwezi moja.

Bi. Fore amesema sasa Yemen kuna medani  49 za kivita na uchumi umevurugika kabisa na familia haziwezi tena kuishi katika hali kama hivyo. Aidha mkurugenzi huyo wa UNCIEF amesema miundo mbinu yote ya Yemen inakaribia kuangamia kikamilifu huku janga la COVID-19 likifanya hali kuwa mbaya zaidi. Halikadhalika amesema wafanya kazi wa kutoa misaada wanakumbana na mzingiro uliowekwa na Saudia dhidi ya Yemen na hivyo ni vigumu kuwafikia mamilioni ya Wayemen wanaohitaji misaada. Amesema watoto  zaidi ya milioni 2.1 wanakabiliwa na lishe duni huku 358,000 wakiwa katika hali mbaya mno.  Afisa huyo wa UNICEF  amesema mustakabali wa mamilioni ya Wayeme umevurugika kutoka na vita nchini humo.

Hivi karibuni pia, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) lilisema kati ya Januari na Juni 2021, asilimia 54 ya Wayemen, yaani watu milioni 16.2, watakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.

Aidha mapema mwezi huu wa Disemba,  Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) ilitangaza kuwa vita vya Saudi Arabia dhidi ya Yemen vimepelekea zaidi ya watu 233,000 kupoteza maisha katika kipindi cha miaka sita iliyopita.

Ikumbukwe kuwa mnamo mwezi Machi 2015 Saudi Arabia, ikiungwa mkono na  Marekani, utawala haramu wa Israel, Umoja wa Falme za Kiarabu  na nchi zingine kadhaa iliivamia kijeshi Yemen na kuiwekea mzingiro wa kila upande.

Utawala dhalimu wa Saudia ulianzisha mashambulizi dhidi ya Yemen mwishoni kwa lengo la kuiondoa madarakani Harakati ya Ansarullah na kumrejesha madarakani kibaraka wake, Abdrabbuh Mansour Hadi, rais wa zamani wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kukimbilia Riyadh. Hata hivyo hadi sasa Saudia na washirika wake wameshindwa kufikia malengo yao kutokana na kusimama kidete wananchi wa Yemen.

3473388

captcha