IQNA

Saudia imekuwa ikitamani sana kuwa na uhusiano na Israel

22:17 - December 05, 2020
Habari ID: 3473426
TEHRAN (IQNA) - Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia ameeleza bayana kuwa kuanzisha uhusiano kamili wa kidiplomasia na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ni sehemu ya ndoto ya muda mrefu ya kisiasa ambayo wamekuwa nayo viongozi wa utawala wa Aal Saud.

Faisal bin Farhan Aal Saud amethibitisha kuwa kwa muda mrefu suala la kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel limekuwa sehemu ya ndoto na matarajio ya Saudia na kwamba mpango huo ulizungumziwa kwa mara ya kwanza mwaka 1982 na mfalme wa nchi hiyo wakati huo Fahad bin Abdulaziz Aal Saud.

Farhan ameongeza kuwa, ndoto na matarajio ya Riyadh ni kuona Israel inaanzisha uhusiano kamili na wa kawadia na nchi jirani na utawala huo wa Kizayuni na kufanyika mazungumzo kati ya Tel Aviv na Wapalestina kwa ajili ya kufikia mapatano.

Pamoja na hayo Faisal bin Farhan Aal Saud amesema, ili Saudia ichukue hatua hiyo ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel yanahitaji kufikiwa kwanza makubaliano ya amani yatakayodhamini kuundwa nchi ya Palestina, yenye hadhi na mamlaka ya kujitawala, ambayo itakubaliwa na Wapalestina wenyewe.

Hivi karibuni pia, alipozungumza pembeni ya kikao cha G20, waziri huyo wa mambo ya nje wa Saudi Arabia alisema, nchi yake siku zote imekuwa ikiunga mkono wazo la kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel na kufikia mapatano ya kuwa na suluhu ya kudumu na utawala huo.

Itakumbukwa kuwa, katika hatua inayopingana kikamilifu na malengo matukufu ya watu wa Wapalestina ya ukombozi wa nchi yao, tarehe 25 Septemba, mawaziri wa mambo ya nje wa Imarati na Bahrain walisaini mkataba wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel katika hafla iliyofanyika Ikulu ya White House mjini Washington na kuhudhuriwa na rais wa Marekani Donald Trump na waziri mkuu wa utawala haramu wa Israel Benjamin Netanyahu. 

Hatua hiyo ilikosolewa na kulaaniwa vikali na viongozi wa Palestina, wakisema kuwa ni sawa ni kulichoma jambia la mgongo piganio tukufu la Palestina na watu wake.

3939083

Kishikizo: saudia israel palestina
captcha