IQNA

Mwanazuoni wa Lebanon

Ni Haramu kuwa na uhusiano wa kawaida na Israel

22:00 - December 06, 2020
Habari ID: 3473429
TEHRAN (IQNA) – Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu wa Madhehebu ya Shia Lebanon Ayatullah Abdul-Amir Qabalan amelaani vikali jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina Waislamu na Wakristo na kuongeza kuwa, kuanzisha uhusiano na Israel ni haramu.

Ayatullah Qabalan ameongeza kuwa, si tu kuwa kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel ni usaliti kwa umma wa Kiislamu bali ni kufungua njia kwa utekelezwaji wa ule mkataba wa 'muamala wa karne' uliowasilishwa na Marekani kwa lengo la kuangamiza harakati za ukombozi wa Palestina.

Aidha Ayatullah Qabalan amelaani jaribio la hivi karibuni la Muisraeli kuteketeza moto kanisa katika mji wa Quds (Jerusalem) na kusema hiyo ni ishara ya uhasama wa Wazayuni kwa maeneo matakatifu ya Waislamu na Wakristo. Ametoa wito kwa Waislamu na Wakristo kuungana katika kukabiliana na itikadi chafu ya Wazayuni.

Itakumbukwa kuwa, katika hatua inayopingana kikamilifu na malengo matukufu ya watu wa Wapalestina ya ukombozi wa nchi yao, tarehe 25 Septemba, mawaziri wa mambo ya nje wa Imarati na Bahrain walisaini mkataba wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel katika hafla iliyofanyika Ikulu ya White House mjini Washington na kuhudhuriwa na rais wa Marekani Donald Trump na waziri mkuu wa utawala haramu wa Israel Benjamin Netanyahu.  Sudan pia imefuata mkumbo huo na kutangaza utayarifu wa kuanzisha uhusiano na utawala huo bandia.

Hatua hiyo ilikosolewa na kulaaniwa vikali na viongozi wa Palestina, wakisema kuwa ni sawa ni kulichoma jambia la mgongo piganio tukufu la Palestina na watu wake.

 3939443

captcha