IQNA

Wairaqi waandamana kukumbuka kuuawa shahidi Qassem Soleimani na Al-Muhandis

12:35 - December 27, 2020
Habari ID: 3473496
TEHRAN (IQNA)- Watu wa Iraq wameandamana katika mji mkuu, Baghdad, kulaan kitendo cha kigaidi cha Marekani cha kuwaua makamanda wakuu wa vita dhidi ya ugaidi, Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani na mwanamapmabano mwenza wa Iraq Abu Mahdi al Muhandis.

Maandamano hayo ambayo yamefanyika katika Medani ya Tahrir mjini Baghdad ikiwa inakaribia mwaka moja tokea Marekani itekeleza hujuma ya kigaidi iliyopelekea makamanda hao kuuawa.

Katika maandamano hayo ambayo aghalabu ya washiriki wake walikuwa ni wanamapambano wa Jeshi la Kujitolea la Wananchi maarufu kama Hashd al Sha’abi waandamnaji wamelaani vikali ugaidi wa Marekani .

Luteni Jenerali Qassem Soleimani aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) alielekea Iraq kufuatia mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo aliuawa shahidi tarehe 3 Januari mwaka huu katika shambulio la anga la wanajeshi vamizi na magaidi wa Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad Iraq akiwa pamoja na Abu Mahdi al Muhandis Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq (Hashdu Shaabi) na wenzao wanane. Kamanda Soleimani alikuwa safarini nchini Iraq kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo.

3473515

Kishikizo: iraq Soleimani irgc
captcha