IQNA

Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza wamemuenzi Shahidi Soleimani

17:27 - December 29, 2020
Habari ID: 3473505
TEHRAN (IQNA) – Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza wamemuenzi Shahidi Luteni Jeneali Qassem Soleimani mwaka mmoja baada ya kuuawa kwake katika hujuma ya jeshi la kigaidi la Marekani katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad.

Katika mahojiano na Press TV, Wapalestina katika ukanda huo wa pwani wamesema Shahidi Qassem Soleimani alijitolea muhanga maisha yake kwa ajili ya kukkabiliana na utawala dhalimu wa Israel ili kukomboa Palestina na hasa mji mtakatifu wa Quds au Jerusalem.

Wamesema Shahidi Qassem Soleimani daima aliunga mkono mapambano ya Wapalestina dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Baada ya kuuawa shahidi Qassem Soleiamni Januari mwaka huu, Wapalestina wameandaa hafla kadhaa za kumuenzo mwanamapambano huyo. Wapalestina wanamtazama Qassem Soleimani kama shujaa wa Palestina na Quds Tukufu.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) alielekea Iraq Januari 3 mwaka 2020 kufuatia mwaliko rasmi wa wakuu wa Iraq. Punde baada ya kuwasili Iraq aliuawa shahidi katika hujuma ya ndege za kivita za jeshi vamizi na la kigaidi la Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad. Aidha katika hujuma hiyo ya kigaidi Abu Mahdi Al Muhandis, Naibu Mkuu wa Harakati ya Kujitolea ya Wananchi wa Iraq, naye pia aliuawa shahidi akiwa ameandamana na Qassem Soleimani. Watu wengine wanane waliokuwa katika msafara huo nao pia waliuawa shahidi.

Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani mbali na kuunga mkono harakati za ukombozi wa Palestina pia alikuwa na nafasi kubwa katika mapambano na maadui pamoja na magaidi na pia katika kuangamiza kundi la kigaidi la Daesh au ISIS. Halikadhalika alikuwa na nafasi muhimu katika kusambaratisha njama ya Marekani na Wazayuni ya kuligawa eneo vipande vipande.

3473540

captcha