IQNA

Gaidi aliyeua watu 28 mjini Baghdad, Iraq alikuwa raia wa Saudia

21:14 - January 21, 2021
Habari ID: 3473578
TEHRAN (IQNA)- Maafisa wa Iraq wamesema rais wa Saudi Arabia ni mmoja kati ya magaidi waliotekekeleza hujuma iliyopelekea raia 28 wasio na hatua kuuwa mjini Baghdad.

Abbas Zaidi mmoja wa wakuu wa Jeshi la Kujitolea la Wananchi wa Iraq maarufu kama Hashd al Shaabi amesema: ‘Imebainika kuwa mmoja wa magaidi waliojirupua katika kati ya mji wa Baghdad alikuwa ni raia wa Saudi Arabia.”

Hadi sasa waliojeruhiwa katika hujuma hiyo ya ya kigaidi karibu na Medani ya al Tayran wamepindukia 110.

Brigedia Jenerali Hazem al Azzawi Mkurugenzi wa Kamandi ya Oparesheni ya Baghdad ameliambia shirika la habari la Iraq (INA) kuwa, milipuko pacha imetokea katika soko lenye watu wengi katika eneo la Bab al Sharji karibu na Medani ya al Tayran.  

Wakati huo huo, ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huko Baghdad umetoa taarifa ukitoa mkono wa pole kwa familia za wahanga wa jinai hiyo ya kigaidi na kuwatakia pia majeruhi wa milipuko hiyo shifaa ya haraka.

Taarifa ya ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huko Baghdad aidha imeunga mkono hatua za serikali na vyombo vya usalama vya Iraq na kusisitiza kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kama ilivyo siku zote inasisitiza kuiunga mkono serikali na wananchi wa Iraq na iko tayari kutoa msaada wowote unaohitajika. 

Ubalozi wa Iran mjini Baghdad umesema unataraji kuwa vyombo vya usalama vya Iraq vitawatia nguvuni wahusika wakuu wa milipuko hiyo na kuwaadhibu.

 

3949087

Kishikizo: iraq ugaidi saudia
captcha