Tukio hilo lilifanyika katika Msikiti wa Umayyad, Msikiti wa Al-Hamza, na Msikiti wa Al-Abbas huko Damascus, ambapo wahifadhi wa Qur’ani walishindana kukamilisha Qur’ani nzima kwa kusoma katika kipindi kimoja, kuanzia saa 11 alfajiri hadi saa 2 usiku.
Kulingana na Mohammad Joweid, Mkurugenzi wa Masuala ya Qur’ani katika Wizara ya Wakfu, lengo la mashindano hayo lilikuwa “kukuza utamaduni wa Qur’ani na kufufua nafasi ya misikiti kama vituo vya ibada na elimu.”
“Jumla ya wanaume 163 na takriban wanawake 500 wenye umri wa miaka 12 hadi 35 walijiandikisha kushiriki, baada ya kufuzu kupitia mtihani maalum,” aliongeza.
Abdul Qader Barakat, mkuu wa Masuala ya Qur’ani Damascus, alisisitiza upekee wa tukio hilo, akisema: “Hili lilikuwa shindano la kwanza kabisa nchini Syria la kukamilisha Qur’ani yote kwa kikao kimoja, na kwa baraka za Mwenyezi Mungu, limefanyika kwa mafanikio.” Alibainisha idadi kubwa ya wanawake waliohudhuria katika misikiti ya Al-Hamza na Al-Abbas.
Sheikh Mahmoud Al-Ahmad Bek, Mkurugenzi wa Masuala ya Qur’ani katika eneo la Rif Damascus, alithibitisha kwamba washiriki 50 wa kiume na 80 wa kike walihifadhi Qur’ani.
3493173