
Sheikh Naeem Qassim, ameongezea kwa kusema: "Inapasa kupigana Jihadi ili kukabiliana na batili na kuishinda. Sisi hatutasalimu amri na hatutashindwa, na hatutakubali kutawaliwa na batili".
Katibu Mkuu wa harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Lebanon ameendelea kueleza kwamba: Rais wa Marekani Donald Trump anataka kufanya mauaji ya kimbari ya kisiasa kwa kushirikiana na Netanyahu (waziri mkuu wa utawala ghasibu), aliyefanya mauaji ya kimbari ya watu katika Ukanda wa Ghaza lakini akashindwa. Amesema, misimamo ya Trump kuhusu kadhia ya Palestina ni hatari sana kwa sababu anataka kuiangamiza moja kwa moja Palestina na watu wake.
Sheikh Naim Qassem amebainisha kuwa tangu wakati alipouawa shahidi Sheikh Ragheb Harb hadi wakati wa mauaji ya Shahidi Sayyid Abbas Mousavi, Muqawama umepiga hatua kubwa sana. Makamanda Mashahidi walipiga hatua kwa kufuata njia ya Uislamu wa asili wa Nabii Muhammad SAW. Njia yao ni njia ya Muqawama wa Kiislamu na Jihadi dhidi ya Israel ilikuwa ndicho kipaumbele cha makamanda waliouawa shahidi.
Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amezungumzia mpango wa Rais wa Marekani dhidi ya wananchi madhulumu wa Ghaza na kusisitiza kuwa: misimamo ya Donald Trump katika kadhia ya Palestina ni hatari sana na anachotaka ni kuifuta kikamilifu kadhia ya Palestina katika ngazi ya kisiasa.
Ameongezea kwa kusema: "mipango ya Trump (kuhusu Palestina) ni ndoto na udhanifu na haiwezi kutekelezeka".
Halikadhalika, Sheikh Naeem Qassim amesema mpango huo wa Marekani ni hatari kwa nchi za Kiarabu na Kiislamu na akabainisha kuwa: kimya kilichoonyeshwa kimataifa wakati wa vita vya karibuni kimeihamasisha Marekani.
3491887