IQNA

Walowezi wa Kizayuni wauhujumu Msikiti wa Al-Aqsa

22:44 - February 08, 2021
Habari ID: 3473634
TEHRAN (IQNA) – Makumi ya walowezi wa Kizayuni wameuhujumu na kuuvunjia heshima Msikiti wa Al-Aqsa katika eneo la Quds (Jerusalem) mashariki Jumatatu.

Katika taarifa,  Idara ya Wakfu ya Mji wa Quds imesema makumi ya walowezi wa Kizayuni  wakiwa wanalinda na wanajeshi wa Israel wameuhujumu Msikiti wa Al-Aqsa  leo asubuhi wakipitia lango la Al Mughrabah.

Mwezi uliopita, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ilitahadharisha kuhusu mpango wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa kubomoa sehemu za Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem).

Hamas imesema kuwa Wapalestina wako tayari kulinda eneo hilo takatifu hata kama itabidi watoe uhai wao mhanga katika kulinda qibla hicho cha kwanza cha Waislamu.

Aidha Hamase imetoa wito kwa Waarabu na Waislamu kote duniani kujitokeza katika kuutetea Msikiti wa Al Aqsa.

Katika miaka ya hivi karibuni, utawala wa Kizayuni wa Israel umeshadidisha hujuma na uvamizi wake dhidi ya maeneo ya Wapalestina ukifanya njama za kufikia malengo yake haramu katika ardhi za Wapalestina.

Msikiti wa al-Aqsa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu umekuwa ukiandamwa na njama mtawalia za utawala vamizi wa Israel, hatua ambazo zinakwenda sambamba na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina.

3473929

captcha