IQNA

21:22 - February 26, 2021
Habari ID: 3473686
TEHRAN (IQNA)- Umoja wa Mataifa umeutaka utawala wa Kizayuni wa Israel usitishe hatua zake zilizoratibiwa na kubomoa nyumba za Wapalestina.

Lyn Hastings Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu amesisitiza kuwa, Israel inapaswa kusitisha mara moja mipango na operesheni zake zote za kubomoa  na kuharibu nyumba za Wapalestina na mali zao. 

Akizungumza baada ya kutembelea eneo la Hamsa al-Baqi'ah lililoko kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, afisa huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa mwezi huu wa Februari pekee kumeripotiwa matukio matano katika eneo hilo ya kubomolewa nyumba na kuporwa mali na milki za Wapalestina.

Njama hizo za Israel zinakwenda sambamba na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni huko Palestina.

Desemba 23, 2016 Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio 2334 ambalo liliutaka utawala haramu wa Israel usimamishe haraka na kikamilifu shughuli zote za ujenzi wa vitongoji katika ardhi za Palestina unazozikalia kwa mabavu.

Utawala wa Kizayuni ambao unaungwa mkono kikamilifu na Marekani katika hatua zake hizo haramu umedhamiria kubadilisha muundo wa kijiografia na kidemografia wa maeneo ya Palestina; ili kwa kuyazayunisha maeneo hayo, kuhakikisha unazihodhi na kuzidhibiti kikamilifu ardhi za Wapalestina.

Karibu jamii nzima ya kimataifa inasisitiza kuwa hatua ya Israel kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi ni kinyume cha sheria.

3474088

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: