IQNA

Saudia yawafuta kazi maimamu 1000 wanaoupinga ufalme

21:07 - April 02, 2021
Habari ID: 3473777
TEHRAN (IQNA)- Utawala wa Kifalme Saudi Arabia umewafuta kazi maimamu na wahubiri wapatao 1,000 katika misikiti ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa mpinzani maarufu Saudia Yahya al-Assiri, kamatakamata na wahubiri na maimamu ingali inaendelea kote katika nchi hiyo.

Al Assiri amesema sababu kuu ya kufutwa maimamu na wahubiri ni kuwa wanapinga sera za ufalme wa Saudi Arabia.

Baadhi ya wanaharakati wa kijamii wamechapisha orodha ya wahubiri ambao wamefutwa kazi kwa kutaka ususiwaji wa bidhaa za Ufaransa baada ya serikali ya Ufaransa kuunga vitendo vya kuvunjiwa heshima matukufu ya Kiislamu.

Saeed bin Nasser al Ghamdi, mhadhiri wa chuo kikuu ambaye anapinga vikali utawala wa kifalme Saudia, naye pia amechapisha orodha ya wahubiri 50 ambao wamefutwa kazi katika mji mtakatifu wa Makka.

Ufalme wa Saudia haustahamili hata kidogo wahubiri na maimamu wa misikiti ambao wanapinga sera mpya za ufalme huo za kukumbatia utamaduni wa kifasiki wa Magharibi na pia kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel.

3962005

captcha