IQNA

Taarifa kuhusu hali ya kiafya ya Sayyid Hassan Nasrallah baada ya uvumi

18:15 - May 28, 2021
Habari ID: 3473954
TEHRAN (IQNA) – Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema hali jumla ya kiafya ya kiongozi wa harakati hiyo, Sayyid Hassan Nasrallah ni nzuri.

Katika taarifa, Sheikh Naim Qassim, Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah amesema Sayyid Nasrullah alikuwa ameugua na hivyo akawa anahitaji kupumzika. Taarifa hiyo imetolewa baada ya Wazayuni kueneza uvumi kuhusu hali ya kiafya ya kiongozi huyo wa Hizbullah.

Sheikh Naim Qassim amesema: "Katika kipindi cha siku chache zilizopita, Sayyid Nasrullah alikuwa mgonjwa na ili kupata ahueni alihitaji kupumuzika kwa muda wa siku mbili au tatu lakini kwa sababu maashiqi au wapenzi wake walikuwa wanataka kumuona tarehe 25 Mei, alihutubu kwa njia ya televisheni. Kutokana na kuwa kutohutubu kwake katika siku hiyo kungeibua maswali alisisitiza kuwa atahutubu ili awe pembizoni mwa marafiki zake waliokuwa wanasuburi kwa hamu hotuba yake."

Wakuu wa kijeshi na kiusalama katika  utawala wa Kizayuni wa Israel walidai kuwa, kwa mujibu wa walivyomtazama Sayyid Nasrallah akihutubu, alikuwa ameambukizwa corona kutokana na kuwa alikohoa wakati wa hotuba yake.

Sayyed Hassan Nasrallah alihutubu kwa njia ya televisheni Jumanne usiku, ikiwa ni hotuba yake ya kwanza tokea harakati za Palestina zitangaze ushindi katika vita na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Ghaza. Aidha ametoa hotuba hiyo kwa mnasaba wa Siku ya Kitaifa ya Mapambano na Ukombozi. Katika siku hii Walebanon huadhimisha ushindi wao dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel mwaka 2000.

Katika hotuba hiyo, Sayyed Hassan Nasrallah aliuonaya utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa hujuma dhidi ya maeneo matukufu katika mji wa Quds (Jerusalem) inaweza kupelekea kuibuka vita vya kieneo na kuangamizwa utawala huo wa Kizayuni.

Aidha alisema ushindi wa Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza umewashangaza marafiki na maadui. Ameongeza kuwa utawala wa Israel ulikosea katika mahesabu yake huku akipongeza harakati za mapambano ya Kiislamu au muqawama Palestina kwa kusimama kidete dhidi ya Wazayuni.

3974150

captcha