IQNA

Malaysia yazindua mfuko wa kuunga mkono Palestina

22:00 - May 29, 2021
Habari ID: 3473958
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Masuala ya Kidini Malaysia Zulkifli Mohammad al Bakri amesema nchi yake inalenga kuanzisha mfuko maalumu wa kifedha maalumu kwa lengo la kuwasaidia Wapalestina.

Amesema mfuko huo utasimamiwa na  Idara ya Ustawi wa Kiislamu Malaysia kwa ushirikiano na taasisi kadhaa zisizo za kiserikali.

Ameongeza kuwa mfuko utakuwa na jukumu la kuwasaidia Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza na Ukingo wa Magharibi na hivyo ametoa wito kwa Wamalysia wote kuchangua mfuko huo kama njia ya kuonyesha kufungamana kwao na taifa la Palestina.

Siku ya Ijumaa Waziri Mkuu wa Malaysia Muhyiddin Yassin alizungumza na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kuhusu masuala mbali mbali ya Palestina na hujuma ya hivi karibuni ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya raia Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza.

Katika mazungumzo hayo Yassin alisisitiza kuhusu utawala haramu wa Israel kuacha kukalia kwa mabavu ardhi za Palestina.

3974259

captcha