IQNA

19:57 - May 31, 2021
Habari ID: 3473965
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa ulinzi wa Iran amesema Wapalestina waliibuka ushindi hivi karibuni katika vita na utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na imani yao kwa Mwenyezi Mungu kwa Allah SWT.

Akizungumza Jumapili mjini Tehran, Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Brigedia Jenerali Amir Hatami aliashiria ushindi wa wapiganaji wa Wapalestina dhidi ya "utawala wa Kizayuni wa Israeli uliojizatiti kwa kila aina ya silaha," na kusisitiza kuwa, watu wa Palestina walipambana na adui chini ya hali ngumu zaidi "na wakaibuka washindi mbele ya batili  kutokana na imani yao kwa Mwenyezi Mungu.

Aidha amesema  makombora na ndege zisizo na rubani za Palestina zitaendelea kuwa jinamizi walowezi haramu wa Israeli katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu kufuatia uvamizi wa utawala haramu wa Israel ulioshindwa hivi karibuni katika vita dhidi ya Ukanda wa Ghaza.

"Kuanzia sasa, makombora, ndege zisizo na rubani na uwezo wa kujihami wa wamiliki (wa kweli) wa Palestina yatawasumbua walowezi [Waisraeli] kama jinamizi," Brigedia Jenerali Hatami aliuambia mkutano wa maafisa wa ngazi ya juu wa Wizara ya Ulinzi ya Iran.

Aliongeza kuwa mafanikio muhimu zaidi ya ushindi dhidi ya utawala wa Israeli katika vita vya hivi karibuni ni kuimarishwa umoja na mshikamano kati ya Wapalestina wote katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu mbele ya utawala utendao jinai wa Kizayuni na waitifaki wake wa Ulaya na Marekani.

"Kama alivyosema  Kiongozi mwenye busara wa Mapinduzi ya Kiislamu [Ayatollah Seyyed Ali Khamenei] alisema, utawala wa Kizayuni hautaona miaka 25 ijayo," aliongeza Waziri wa Ulinzi wa Iran.

Kuanzia tarehe 10 mwezi wa Mei utawala wa Kizayuni wa Israel ulifanya mashambulizi makubwa ya pande zote dhidi ya Ukanda wa Ghaza huko Palestina kwa muda wa siku 12 na kufanya uharibifu mkubwa sambamba na kuua na kujeruhi idadi kubwa ya Wapalestina wasio na hatia. Utawala wa Kizayuni wa Israel ulilazimika kuchukua hatua ya upande mmoja ya kusitisha vita baada ya kukabiliwa na wimbi la makombora ya Wapalestina waliokuwa wakilipiza kisasi jinai wanazotendewa.

3974530

 

Kishikizo: iran ، hatami ، palestina ، israel ، ghaza
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: