IQNA

Balozi Salah al Zawawi

Vita vya siku 12 Ghaza ni ndio mwanzo wa kuangamizwa kikamilifu utawala wa Israel

18:08 - May 30, 2021
Habari ID: 3473961
TEHRAN (IQNA)-Balozi wa Palestina nchini Iran amesema kuwa, vita vya siku 12 vilivyomalizika hivi karibuni baina ya utawala wa Kizayuni na wanamapambano wa Palestina, vimefungua mlango wa kuangamizwa kikamilifu Israel.

Salah al Zawawi amesema hayo hapa Tehran na kuongeza kuwa, kama alivyokuwa akiamini Imam Khomeini MA, suala la kuangamizwa utawala wa Kizayuni ni kitu kisichoepukika na kwamba vita vya siku 12 ndio mwanzo wa kuangamizwa kikamilifu utawala huo pandikizi.

Vile vile amesema ni jukumu la nchi za Waislamu kuwa bega kwa bega na Palestina kwani bila ya msaada na uungaji mkono wa nchi hizo, muqawama wa taifa la Palestina haotufanikiwa.

Ikumbukwe kuwa, juzi Ijumaa, vijana wa Palestina walitangaza kuwa wameanzisha kampeni kubwa iliyopewa jina la  "Mapambazuko" kwa ajili ya kuendeleza muqawama na mapambano ya taifa hiyo na kuendeleza ushindi wa vita vya siku 12 hadi utawala wa Kizayuni wa Israel utakapotimuliwa kutoka katika ardhi zote za Wapalestina.

3973993

Kishikizo: zawawi ، palestina ، ghaza ، israel
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha