Kwa mujibu wa taarifa, qarii huyo maarufu wa Misri alipoteza maisha Jumatano kutokana na maradhi sugu ya muda mrefu.
Sheikh Abdul Halim amezikwa katika mji wa Talkha mkoani Dakahlia kaskazini mashariki mwa Cairo. Watu wa Misri wamemuomboleza katika mitandao ya kijamii ambapo wamemuombea maghufira huku wakisambaza klipu za qiraa yake.