IQNA

Kamanda Mkuu wa IRGC

Mafanikio ya kisayansi Iran yamepatikana kwa kutegemea mantiki ya Qur’ani Tukufu

21:57 - June 27, 2021
Habari ID: 3474046
TEHRAN (IQNA)- Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema mafanikio ya Iran katika uga wa sayansi yametokana na kutegemea mantiki ya Qur’ani Tukufu.

Meja Jenerali Hussein Salami  Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ameyasema hayo leo mjini Tehran alipozungumza katika uzinduzi wa chanjo nyingine ya COVID-19 ya Iran inayojulikana kama ‘Noora’ na kuongeza kuwa, Iran imeweza kupatana mafanikio ya kisayansi pamoja na kuwa imewekewza mzingiro wa kielimu, kiuhcumi na kifedha.

Kuhusu kuzinduliwa chanjo nyingine zinazozalishwa hapa nchini, Mkuu wa Shirika la Dawa na Chakula la Wizara ya Afya ya Iran Muhammad Reza Shanesaz ameeleza kuwa: Chanjo ya "Noora" si chanjo ya mwisho kuzalishwa ndani ya nchi na kwamba Iran inazo chanjo nyingine ambazo zitatangazwa kwa utaratibu maalumu.  

Katika upande mwingine hafla ya uzinduzi wa chanjo ya Sputnik iliyozalishwa hapa nchini Iran pia ilifanyika jana mjini Tehran. 

Iran iko katika mstari ya mbele kuunda chanjo za COVID-19 ambapo mbali na chanjo hizo za Noora na Sputnik,  pia sasa Iran imezalisha chanjo ya COV Iran Barakat ambayo wiki hii imeanza kutumika rasmi. Chanjo  zingine ambazo zimepiga hatua nzuri katika majaribio ni pamoja na Razi Cov Pars, Fakhra na chanjo ya pamoja ya Taasisi ya Chanjo ya Finlay ya Cuba na Taasisi ya Chanjo ya Pasteur ya Iran.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Shirika la Dawa na Chakula la Iran, Dakta Kianoush Jahanpour, Jamhuri ya Kiislamu imejiunga na kundi la nchi chache duniani zinazozalisha chanjo ya ugonjwa wa COVID-19.

Mkuu wa Shirika la Dawa na Chakula katika Wizara ya Afya na Tiba ya Iran amesema kuwa, kwa mujibu wa mpango ulioandaliwa na serikali, hadi kufikia msimu wa vuli wa mwaka huu wa ya Kiirani, watu milioni 60 nchini watakuwa wamepewa chanjo dhidi ya virusi vya COVID-19..

3980296

Kishikizo: iran Corona covid 19
captcha