IQNA

Waislamu Dunianii

Msikiti wa Kwanza wa Cuba Kujengwa Havana

21:50 - September 20, 2022
Habari ID: 3475815
TEHRAN (IQNA) - Msikiti wa kwanza wa Cuba utajengwa katika mji mkuu Havana ambapo inatarajiwa kuwa ujenzi wake utafadhiliwa na Saudia Arabia kwa ajili ya Waislamu wanaoishi katika nchi hiyo ya Amerika Kusini.

Hayo yametangazwa na balozi wa Cuba jijini Riyadh, Saudi Arabia Vladimir Gonzalez.

"Kwa sababu ya mchango huu kutoka upande wa Saudi, leo tunaweza kusema kwamba tunajenga Havana msikiti wa kwanza katika nchi yetu," Gonzalez alisema katika mahojiano na televisheni ya Saydia.

“Tuna jumuiya ndogo ya Waislamu katika nchi yetu; wamejipanga sana. Nina fahari kuwezesha maisha yao kama Waislamu nchini Cuba.”

Uhusiano wa kidiplomasia wa Cuba na Saudi Arabia ulianza 1956.

"Saudi Arabia ilikuwa taifa la kwanza la Kiarabu kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Cuba," Gonzalez alisema.

Waislamu ambao ni wachache sana Cuba, hadi sasa, wamekuwa wakisali nyumbani au katika maeneo ya ya muda ya sala.

Mfuko wa Maendeleo wa Saudi umeruhusu kuanzishwa kwa miradi ya "kijamii na kiuchumi" ambayo itafaidi mataifa hayo mawili, Gonzalez alisema.

3480560

Kishikizo: cuba ، waislamu ، msikiti
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha