Taarifa zinasema malipuko wa mtungi mkubwa wa oxijeni katika kituo hicho cha matibabu ya corona ndio chanzo cha mtoto huo.
Kufuatia mkasa huo, serikali ya Iraq imetangaa siku tatu za maombolezo ya kitaifa.
Baadhi ya vyombo vya habari Iraq vinasema walioathirika ni wafanyakazi wa sekta ya afya wakiwemo wauguzi na pia maafisa wa zima moto.
Waziri Mkuu wa Iraq Mustafa al Kadhimi amefika katika mji wa Nasiriya kwa ajili ya kufuatialia hali ya mambo baada ya mkasa huo.
Spika wa Bunge la Iraq Mohammad al Hakbousi ameandika katika ukursa wa Twitter kuwa ataitisha kikao cha dhararu leo kwa lengo la kuchunguza maafa hayo ya moto.
Huku ukiwa umeharibiwa na vita na vikwazo, mfumo wa afya wa Iraq umekuwa ukipambana kukabiliana na janga la virusi vya corona ambalo limewaua watu 17,592 na wengine zaidi ya milioni 1.4 wakiwa wameambukizwa.