IQNA

Jinai za Israel

Msikiti wa Ukingo wa Magharibi Wachomwa moto na walowezi wa Kizayuni

19:07 - December 20, 2024
Habari ID: 3479925
IQNA - Kundi la walowezi haramu wa Kizayuni wa utawala haramu Israel wamechoma moto Msikiti wa Bir Al-Walidain katika kijiji cha Marda, kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.

Walioshuhudia walisema kundi la walowezi haramu walivamia kitongoji cha mashariki cha Marda, karibu na mji wa Salfit, na kuuchoma moto msikiti huo kwa makusudi siku ya Ijumaa.

Wakazi walifanikiwa kuzima moto huo, lakini moto huo tayari ulikuwa umesababisha uharibifu mkubwa kwa muundo wa msikiti huo.

Kijiji cha Marda kiko karibu na makazi haramu ya Ariel na kimezungukwa na uzio wa nyaya.

 Pia walowezi hao wameandika maandishi ya Kiibrania yenye chuki kwenye kuta za msikiti huo kama vile 'Mauti kwa Waarabu"

Ghasia za walowezi zimeongezeka kwa kiasi kikubwa tangu tarehe 7 Oktoba 2023, na zaidi ya matukio 1,000 ya uvamizi yalisajiliwa kufikia Septemba 2024 ambapo zaidi ya Wapalestina 1,300 wamefukuzwa kutoka kwa makazi yao.

3491125

captcha