IQNA

22:24 - July 15, 2021
Habari ID: 3474101
TEHRAN (IQNA)- Uchunguzi wa maoni umebaini kuwa, robo ya Mayahudi wa Marekani wanaamini kuwa Israel ni utawala wa ubaguzi wa rangi.

Matokeo hayo ya uchunguzi wa maoni yanaonyesha wazi kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel unapoteza umaarufu hata miongoni mwa Mayahudi.

Uchunguzi huo wa maoni ambayo umetangazwa Jumatano ulifanyika baada ya vita vya siku 11 vya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ukanda wa Ghaza mwezi Mei ambapo Wapalestina zaidi ya 250 wakiwemo wanawake na watoto waliuawa.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo asilimia 25 ya Mayahudi Wamarekani waliafiki kuwa Israel ni utawala wa ubaguzi wa rangi au apathaidi huku asilimia 22 wakikubaliana na taarfia kuwa Israel inatekeleza mauaji ya umati dhidi ya Wapalestina.

Aidha uchunguzi huo umebaini kuwa vijana wengi Mayahudi hawaungu mkono utawala bandia wa Israel. Asilimia 20 ya vijana Mayahudi walio chini ya umri wa miaka 40 wanaamini kuwa , ‘Israel haina haki ya kuwepo.

Uchunguzi huo wa maoni umefadhiliwa na Kituo cha Upigaji Kura cha Mayahudi na kutekelezwa na shirika la GBAO Strategies kati ya Juni 28 na Julai 1.

Matokeo hayo ya uchunguzi wa maoni yamewatia wasiwasi mkubwa viongozi wa Kiyahudi wanaounga mkono utawala haramu wa Israel ambao sasa wanasema wana kibarua kiggumu kukinaisha kizazi kipya cha Mayahudi kuhusu kuunga mkono utawala wa Israel.

3475251

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: