IQNA

20:33 - July 24, 2021
News ID: 3474123
TEHRAN (IQNA) - Wizara ya Maswala ya Kidini ya Algeria imelaani mauaji ya imamu wa msikiti katika mkoa wa kaskazini wa Tizi Ouzou wakati akisali Sala ya Alasiri jioni msikitini.

Kulingana na IQNA, Wizara ya Maswala ya Kidini ya Algeria ililaani mauaji ya imamu wa msikiti katika mkoa wa kaskazini wa Tizi Ouzou na ikatoa taarifa kuelezea tukio hilo la jana  kuwa la kusikitisha na kusisitiza kuwa linafuatiliwa kisheria.

Taarifa hiyo ilisema: "Wizara ya Dini ya Algeria inaelezea msaada wake na mshikamano na familia ya marehemu Hamoudi Bilal na inatoa pole zake.”

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Algeria ilisisitiza kuwa mshambuliaji huyo alikuwa amelazwa hospitalini mara kadhaa katika hospitali ya magonjwa ya akili kulingana na ushuhuda wa raia, na kwamba kwa sasa amekamatwa na kuhojiwa.

Marehemu Hamoudi alikuwa alikuwa mfanyakazi wa Idara ya Masuala ya Dini na alikuwa ameapewa kujukumu la kuswalisha katika Msikiti wa Tariq bin Zayed na alikuwa mhitimu wa Kitivo cha Sayansi ya Kiislamu nchini Tunisia.

3986078

Tags: imamu ، algeria ، msikiti
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: