IQNA

Diplomasia ya Kiislamu

Rais wa Iran atembelea msikiti mkubwa zaidi barani Afrika akiwa Algeria

22:26 - March 03, 2024
Habari ID: 3478444
IQNA-Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametangaza utayarifu wake wa kupanua uhusiano wa kiutamaduni kati ya Iran na Algeria kwa kuzingatia misikiti kama msingi na katika mwelekeo wa kuongeza maarifa, sayansi na kujenga umoja na mafungamano katika ulimwengu wa Kiislamu.

Rais Raisi ameyasema hayo Jumapili alipotembelea sehemu tofauti za msikiti ambao ni mkubwa zaidi Afrika, alikofahamishwa kuhusu mchakato wa ujenzi wake.

Akizungumza msikitini hapo, Raisi ameutaja umoja na mshikamano kuwa ni miongoni mwa mahitaji muhimu zaidi ya ulimwengu wa Kiislamu hivi leo na akasema kuwa, kuunda umoja na mafungamano baina ya Umma wa Kiislamu ni moja ya kazi muhimu za misikiti na ina nafasi yenye ufanisi katika suala hili.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, katika kikao na Imam wa Msikiti wa Jamia wa Algeria, alitaja "kueneza mafundisho ya dini na mafundisho ya Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) na Ahlul-Bayt (AS)", kuzingatia hali ya waumini na umakini wa kutatua shida zao" ni miongoni mwa kazi muhimu za misikiti.

Aidha ameongeza kuwa, leo hii, kupaza sauti ya Waislamu wanaodhulumiwa wa Palestina katika Ukanda wa Gaza, kama suala kuu la ubinadamu, kuwe katikati sehemu ya shughuli za misikiti katika nchi za Kiislamu.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aidha ameeleza kuwa, kwa bahati nzuri Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Algeria zina msimamo mmoja kuhusu suala la Palestina na kusema kwamba, iwapo misimamo hiyo hiyo ya pamoja katika kuliunga mkono taifa madhulumu la Palestina na kukabiliana na utawala wa Kizayuni ingekuwepo  katika ulimwengu mzima wa Kiislamu, je, Wazayuni wangethubutu kufanya wanyaofanya?

Imamu wa Masjid ya Al-Jazair (Msikiti wa Jamia wa Al Jazair) akiwasilisha ripoti ya historia ya ujenzi wa msikiti huu ameashiria njama za Wafaransa kubadilisha dini na imani za taifa la Algeria katika kipindi cha ukoloni na kusema kuwa pamoja na hayo, juhudi za taifa la Algeria bado linafuata kanuni na imani zake lilirudisha uhuru kwa nchi hii na kugeuza mahali pa shughuli za kikoloni za wakoloni kuwa Msikiti Mkuu wa Algeria.

Iranian President Tours Africa’s Largest Mosque during Algeria Visit

Imamu wa Msikiti wa Al Jazair alipongeza misimamo ya kijasiri na ya kihistoria ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusiana na kadhia ya Palestina ameeleza matumaini yake kuwa nchi nyingine za Kiislamu pia zitachukua hatua katika mwelekeo huo.

Msikiti huo mkubwa zaidi barani Afrika, unaochukua waumini 120,000, ulifunguliwa nchini Algeria mwezi uliopita.

Msikiti huo umezinduliwa baada ya miaka mingi ya ujenzi kusimama kutokana na gharama kubwa. Msikiti huo ambao unajulikana kama Djamaa El-Djazair, umejengwa kwa usanifu majengo wa kisasa uuko katika eneo lenye ukubwa wa hekta 27.75 (karibu ekari 70), na unatajwa kuwa wa tatu kwa ukubwa duniani baada ya misikiti miwili huko Makka na Madina, maeneo takatifu zaidi ya Uislamu, huko Saudi Arabia. Ukumbi wake wa swala unaweza kuchukua watu 120,000.

Msikiti Mkuu wa Algiers uliojengwa na kampuni ya ujenzi ya China katika miaka muongo wote wa 2010, pia una mnara mrefu zaidi duniani, wenye urefu wa futi mita 265. Muundo wake wa kisasa umeiga mitindo ya ujenzi ya Kiarabu na Afrika Kaskazini na unanezi mila na tamaduni za Algeria. Msikiti huo una maktaba ambayo inaweza kuhifadhi hadi vitabu milioni 1. Rais wa Algeria Abdelmajid Tebboune alizindua msikiti huo, akitimiza ahadi yake ya kuufungua kwa fahari na hali nzuri.
Msikiti huo awali ulikuwa mradi wa Rais wa zamani hayati Abdelaziz Bouteflika, ambaye alianza ujenzi wake akiwa na nia ya kuufanya uwe mkubwa zaidi barani Afrika.

3487401

captcha