IQNA

Qarii Misri afariki akisoma Qur’ani Tukufu

19:29 - July 31, 2021
Habari ID: 3474143
TEHRAN (IQNA)- Qarii au msomaji wa Qur’ani Tukufu nchini Misri amefariki dunia akiwa anasoma Qur’ani Tukufu.

Kwa mujibu wa tovuti ya El Balad, marhum Sheikh Mohammad Hassan al Fardi alikuwa akisoma aya katika Sura Ar-Rahman katika kikao cha khitma wakati alipofariki katika mkoa wa Sharqiya.

Waliokuwa wamehudhuria khitma hiyo walishtuka walipoona qiraa yake imesita ghafla na walipofika katika Mimbar iliwabainikia kuwa qarii huyo alikuwa amerejea kwa Mola wake.

Sheikh al Fardi alikuwa na umri wa miaka 90 na alikuwa Hafidh wa Qur’ani Tukufu mbali na kuwa na uwezo wa kusoma Qur’ani kwa mbinu saba tafauti. Katika umri wake aliweza kuwaelimisha mamia ya wasomaji Qur’ani aktika kijiji chake na pia maeneo mengine ya jimbo la Sharqiya.

Wengi katika mitandao ya kijamii wametuma salamu za rambi rambi kufuatia kifo cha msomi huyo huku wakimuomba Allah SWT amrehemu.

3987575

 

Kishikizo: misri qarii fardi
captcha